Sha256: 32ec1156658b72ab6baa3e15d43505f6fec24b70659776a145bdf93ac946832f
Contents?: true
Size: 1.55 KB
Versions: 7
Compression:
Stored size: 1.55 KB
Contents
Jina hilo linatumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka yaPapa wa Roma kama mkuu wa Maaskofu juu yake lote. Kanisa hilo linaamini kuwa ndani yake linadumu moja kwa moja Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu Kristo ambalo wanaunganishwa nalo wote wanaobatizwa katika madhehebu yoyote. Tofauti kati yao ni kwamba baadhi (Wakatoliki) wana ushirika kamili nalo, wakati wengine (hasa Waorthodoksi na Waprotestanti) wana ushirika nalo kwa viwango mbalimbali, kadiri wanavyokubali mafundisho,sakramenti na uongozi wake. Neno "katoliki" linatokana na kivumishi cha Kigiriki καθολικός (katholikòs), lenye maana ya «kamili, kadiri ya utimilifu». Kwa mara ya kwanza liliandikwa na Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wa Smirna mwanzoni mwa karne II: «Alipo Yesu Kristo ndipo lilipo Kanisa Katoliki» (Ad Smyrnaeos, 8). Kati ya madhehebu ya Kikristo, Kanisa Katoliki linakusanya waamini 1,166,000,000, yaani nusu ya wafuasi wote wa Yesu, na 17.4 % ya binadamuwote, likiwa na asilimia kubwa ya waamini kati ya wananchi wa Amerika na Ulaya. Kanisa Katoliki linaishi katika majimbo 2,945, ambayo kwa kawaida yanaongozwa na Maaskofu (kwa jumla wako 5,002) wakisaidiwa na mapadri (409,166) na mashemasi; kati ya hayo, mengi yanafuata mapokeo ya magharibi, lakini machache mapokeo ya mashariki. Majimbo yanagawanyika katika parokia zinazoongozwa na padri anayeitwa paroko. Kati ya waamini wana nafasi ya pekee wamonaki na watawa wengine ambao wanaishi kwa mitindo iliyostawi katika historia ya Kanisa ili kumfuata Yesu kwa karibu zaidi katika useja mtakatifu, ufukara na utiifu.
Version data entries
7 entries across 7 versions & 1 rubygems